• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalaani vikali matumizi yoyote ya mabavu dhidi ya ofisi za kidiplomasia

    (GMT+08:00) 2018-11-23 19:02:33

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inalaani vikali matumizi yoyote ya mabavu dhidi ya ofisi za kidiplomasia.

    Geng Shuang amesema hayo baada ya watu watatu wenye silaha leo asubuhi kwa saa za Pakistan kujaribu kuvamia ubalozi mdogo wa China nchini humo na kujibizana kwa risasi na polisi baada ya kugunduliwa na kusababisha vifo vya askari polisi wawili na watu hao watatu.

    Bw. Geng amesema, wafanyakazi wote wa ubalozi huo na jamaa zao wako salama. China imetoa salamu ya rambirambi kwa askari polisi wa Pakistan waliouawa katika mapigano hayo, huku ikiitaka serikali ya Pakistan kuchukua hatua halisi kulinda usalama wa raia na makampuni ya China nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako