• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OECD yapunguza matarajio kwa ongezeko la uchumi wa dunia kwa mwaka kesho.

    (GMT+08:00) 2018-11-23 19:03:09

    Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) limetoa ripoti mpya ya matarajio ya uchumi wa dunia, na kupunguza matarajio kwa ongezeko la uchumi wa dunia kwa mwaka kesho.

    Ripoti hiyo inaonya kuwa, kuongezeka kwa ushuru kwa sababu ya kujilinda kibiashara kutaathiri biashara ya kimataifa na ukuaji wa uwekezaji, na kuongezeka kwa viwango vya riba na thamani ya dola za kimarekani kutasababisha kuondoka kwa mitaji kwenye masoko mapya na kudhoofisha sarafu zao.

    Ripoti hiyo imesema, hatari mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya bei ya mafuta, mashaka kuhusu kama Uingereza itajitoa kutoka Umoja wa Ulaya, na udhaifu wa benki za nchi zinazotumia Euro, zinaathiriana, na huenda zitasababisha ongezeko la uchumi wa dunia kushuka kwa kiasi kikubwa.

    Wakati huohuo, taasisi ya uchumi ya Oxford imetoa ripoti ya utafiti inayosema ukuaji wa uchumi wa dunia wa mwaka 2019 utashuka kutoka asilimia 3.1 ya mwaka huu hadi asilimia 2.8.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako