• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawakilishi wa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanya ziara nchini China

    (GMT+08:00) 2018-11-23 19:21:49

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang hapa Beijing amesema, China, ikiwa mwenyekiti wa zamu wa mwezi wa Novemba wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, itawaalika wawakilishi wa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza hilo, nchi wanachama wateule na nchi zilizopeleka askari katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa pamoja na maofisa waandamizi wa ofisi ya katibu ya umoja huo kufanya ziara ya siku nne nchini China kuanzia jumapili ijayo.

    Bw. Geng amesema, katika ziara hiyo, viongozi wa China watakutana na ujumbe huo, ambao pia utatembelea vikosi vya China vinavyosubiri kutekeleza majukumu ya kulinda amani na mkoa wa Guangdong.

    Ameongeza kuwa anaamini kuwa ziara hiyo itazisaidia nchi wanachama wa Baraza la Usalama kuelewa zaidi njia ya kujiendeleza ya China na sera zake kwa nje, pia itasaidia jamii mbalimbali za China kuufahamu Umoja wa Matiafa na Baraza la Usalama, na kuimarisha ushirikiano na mshikamano kati ya China na nchi wanachama wa Baraza hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako