• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI nchini China yakadiriwa kufikia milioni 1.25 mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-11-23 19:22:14

    Kamati ya afya ya taifa ya China imesema, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu idadi ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI inakadiriwa kufikia milioni 1.25, na njia kuu ya maambukizi ni ngono isiyo salama.

    Takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, idadi ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ilifikia laki 8.5, huku idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ikifikia laki 2.62. Inakadiriwa kuwa idadi ya maambukizi mapya imefikia elfu 80 kila mwaka, ambapo kiwango cha maambukizi kimefikia tisa kwa watu elfu kumi.

    Mtaalamu mkuu wa magonjwa ya mlipuko wa kituo cha kinga na udhibiti wa magonjwa cha China Bw. Wu Zunyou amesema, kwa mujibu wa kigezo cha kimataifa, maambukizi ya UKIMWI ya China bado iko katika kiwango cha juu, lakini maambukizi hayo hayajasambaa kwa uwiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako