• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AMISOM kuandikisha askari polisi wapya nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2018-11-24 16:53:47

    Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imesema inatekeleza mpango kabambe wa kuandikisha askari polisi kwenye jimbo la HirShabelle nchini Somalia ili kuleta utulivu nchini.

    Tume hiyo imefafanua kuwa awamu ya kwanza ya uandikishaji wa maofisa wa polisi itaanza kwa uangalizi, uchunguzi na mafunzo ya takriban polisi wapya 200 walioandikishwa katika mji wa Jowhar. Aidha AMISOM imesema askari wapya watapatiwa kozi ya upolisi ya miezi mitatu, ili kuwapa ujuzi kwenye masuala muhimu ya upolisi, na kudokeza kuwa inafanya kazi kwa ushirikiano na Kikosi cha Polisi cha Somalia kuwajengea uwezo askari wapya ili wapate kutekeleza kwa ufanisi sheria jimboni hapo.

    AMISOM inatarajia kuwaandikisha maofisa 800 wa polisi katika jimbo la HirShebelle pekee, ikiwa kama sehemu ya kukabidhi majukumu ya kuisalama kwa vikosi vya usalama vya Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako