• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya wapiganaji 700 wa zamani wa Rwanda waondoshwa DRC

    (GMT+08:00) 2018-11-24 16:54:38

    Zaidi ya wapiganaji wa zamani wa kundi la waasi la FDLR wapatao 700 wamerejeshwa Rwanda kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, lilipokuwa likikaa kundi hilo.

    Kwenye taarifa yake serikali ya Rwanda imesma kundi jingine lenye wapiganaji zaidi ya 800 linatarajiwa kurejeshwa katika siku za hivi karibuni. Wapiganaji hao pamoja na wake na watoto wao wamepewa vifurushi vya kurejeshwa pamoja na uangalizi wa kiafya katika kituo cha kuwahamasisha na kuwaunganisha na jamii katika wilaya ya Musanze, kaskazini mwa Rwanda, na kwamba watoto wanapatiwa chanjo zote huku wajawazito wakipatiwa huduma za ujauzito.

    Wapiganaji hao wa zamani wamekuwa wakiishi katika kambi mbalimbali za muda mashariki mwa DRC kwa zaidi ya miaka miwili, ambako walikusanywa kama sehemu ya juhudi za pamoja za UN na za kikanda za kuyarejesha makundi ya waasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako