• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN alaani mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyotokea nchini Pakistan

    (GMT+08:00) 2018-11-24 19:02:35

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres alitoa taarifa kupitia msemaji wake akilaani mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyotokea jananchini Pakistan.

    Kwa mujibu wa taarifa, Bw. Guterres alilaani shambulizi dhidi ya ubalozi mdogo wa China huko Karachi nchini Pakistan na shambulizi la kigaidi lililotokea sehemu ya kaskazini magharibi mwa Pakistan, na kutoa salamu za rambirambi kwa jamaa wa watu waliouawa, na kuwaombea majeruhi wapone haraka. Bw. Guterres pia alitoa salamu za pole kwa serikali ya Pakistan na watu wa Pakistan, na kutaka washambuliaji waadhibiwe kisheria.

    Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang , , watu watatu wenye silaha walijaribu kuingia kwenye ubalozi mdogo wa China uliopo Karachi, lakini walipambana na polisi wa Pakistan na kuuawa. Walinzi wawili wa Pakistan waliuawa katika mapambano hayo, na wafanyakazi wote na jamaa zao kwenye ubalozi mdogo wa China huko Karachi wote wako salama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako