• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzoefu wa mageuzi na kufungua mlango wa China unaweza kunufaisha na nchi nyingine

    (GMT+08:00) 2018-11-25 18:06:30

    Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon hivi karibuni amehojiwa na waandishi wa habari wa Shirika la habari la China Xinhua, akisema baada ya China kuanza mageuzi na kufungua mlango mwaka 1978, jamii ya China imepata mabadiliko makubwa, na uzoefu wa maendeleo wa China unastahili kunufaisha nchi nyingine.

    Bw. Ban Ki-moon amesema takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, idadi ya watu maskini duniani imeshuka hadi milioni 836 ya mwaka 2015 kutoka bilioni 1.9 ya mwaka 1990, na malengo ya milenia yametimizwa. Juhudi za China katika kuondoa umaskini zimesaidia Umoja wa Mataifa kutimiza lengo hilo. Sasa China inajitahidi kutimiza lengo la kutokomeza umaskini ifikapo mwaka 2020, lengo hilo litakuwa mafanikio makubwa na litakuwa na umuhimu kwa China na kwa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako