• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika atoa mwito wa kukomesha haraka mgogoro wa Sudan

    (GMT+08:00) 2018-11-25 18:17:26

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahmat amezitaka pande zinazopambana kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan, kutafuta suluhisho la haraka la mgogoro wao uliodumu kwa muda mrefu katika eneo hilo. Bw Mahmat ametoa mwito huo baada ya kufanya mazungumzo na makundi ya SLM na JEM kwenye makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa.

    Kwenye mikutano iliyofanyika tarehe 22 na 23, na viongozi wa makundi ya SLM na JEM, Bw Minni Minawi na Gibril Ibrahim, Bw. Mahmat ameeleza umuhimu wa kumaliza haraka mgogoro huo.

    Kwenye mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na maofisa waandamizi wa umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, Bw. Minawi na Bw. Ibrahim walieleza utayari wa kuanza mazungumzo na serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako