• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la UN latoa taarifa ya mwenyekiti kuhusu kushambuliwa kwa ubalozi mdogo wa China huko Karachi

    (GMT+08:00) 2018-11-25 18:23:02

    Mwenyekiti wa zamu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambaye pia ni balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu, jana huko New York alitoa taarifa ya mwenyekiti akilaani vikali kushambuliwa kwa ubalozi mdogo wa China huko Karachi na kusababisha vifo vya walinzi wawili wa Pakistan.

    Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyotokea tarehe 23 mwezi Novemba nchini Pakistan. Pia zimeipongeza serikali ya Pakistan kujibu kwa haraka, zikitoa salamu za pole kwa jamaa wa watu waliouawa na serikali ya Pakistan, na kuwatakia majeruhi wapone haraka.

    Nchi wajumbe wa baraza la usalama zimesisitiza kuwa ugaidi wa aina zote unatishia amani na usalama wa kimataifa, na inapaswa kuchukua hatua zote kupambana na vitendo vya kigaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako