• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya wapitisha makubaliano ya Brexit ya Uingereza

    (GMT+08:00) 2018-11-25 19:42:16

    Viongozi wa Umoja wa Ulaya leo kwenye mkutano maalumu wa Umoja huo mjini Brussels, wamepitisha rasmi makubaliano ya Brexit yaliyofikiwa na Umoja wa Ulaya na Uingereza. Hayo ni matokeo makubwa yaliyopatikana baada ya Uingereza na Umoja wa Ulaya kuanzisha mazungumzo ya Brexit.

    Mwenyekiti wa baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk‎ ametangaza habari hiyo kwenye vyombo vya habari vya kijamii akisema, viongozi wa nchi wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya wamepitisha nyaraka mbili za kisiasa za makubaliano ya Brexit, na taarifa ya uhusiano kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya katika siku za mbele.

    Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Uingereza italipa paundi bilioni 39 kwa Umoja wa Ulaya, na kuweka kipindi cha miezi 21 ya mpito kuanzia mwezi Machi mwaka kesho, ambapo Uingereza itaendelea kubaki katika soko la pamoja la Ulaya na muungano wa ushuru wa Umoja wa Ulaya, na kufanya biashara bila ushuru.

    Makubaliano hayo pia yanasema Uingereza na Umoja wa Ulaya zitajenga eneo la biashara huria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako