• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sadio Mane amwaga wino Liverpool, Jurgen Klopp amwagia sifa

    (GMT+08:00) 2018-11-26 08:58:07
    Nyota wa klabu ya Liverpool, Sadio Mane amekubali kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya miamba hiyo ya soka ya England. Mane mwenye umri wa miaka 26 amekubali kandarasi hiyo itakayo mfanya kuendelea kuwepo Anfield hadi mwaka 2023.

    Meneja wa timu hiyo, Jurgen Klopp amemwagia sifa nyota huyo kwakusema kuwa hakuna klabu yoyote barani Ulaya ambayo haitaji aina ya mchezaji kama Sadio.

    Mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal amefunga jumla ya mabao 40 kwenye michezo yake 89 aliyocheza Liverpool tangu aliposajiliwa akitokea Southampton kwa dau la pauni milioni 34 mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako