• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo kutokana na ajali ya boti Uganda yafikia 35

    (GMT+08:00) 2018-11-26 08:58:14

    Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Luteni kanali Deo Akiiki amesema idadi ya vifo kutokana na ajali ya kupinduka kwa boti iliyotokea wikiendi ilyopita kwenye ziwa Victoria, katikati ya Uganda, imefikia 35.

    Msemaji huyo ameliambia Shirika la habari la China Xinhua kuwa operesheni za uokoaji na utafutaji wa miili, zitaendelea kwa wiki moja au zaidi lakini kuna uwekezano mdogo wa kuwapata walionusurika.

    Polisi nchini Uganda wamesema boti mbili zilipinduka na kuzama karibu na kisiwa cha Mutima usiku wa Jumamosi, kutokana na kubeba watu kupita kiasi na hali mbaya ya hewa.

    Kwa mujibu wa polisi, mpaka sasa watu 27 wameokolewa, na vyombo vya habari vya huko vimeripoti kuwa kulikuwa na watu zaidi ya 120 kwenye boti hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako