• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Afrika Kusini kutoa hati ya kiapo ya kupinga ombi la mahakama juu ya mageuzi ya ardhi

    (GMT+08:00) 2018-11-26 08:58:36

    Msemaji wa bunge la Afrika Kusini Bw. Moloto Mothapo amesema bunge la nchi hiyo limetoa hati ya kiapo ya kupinga ombi moja la mahakama la kutaka kuweka kando ripoti juu ya marekebisho ya katiba yanayotandika njia kwa ajili ya mageuzi ya ardhi.

    Bw. Mothabo amesema, hati hiyo ya kiapo imetolewa kujibu ombi lililowasilishwa na Shirika la kiraia la AfriForum kwa Mahakama ya juu ya Cape magharibi, linalotaka kuwekwa kando kwa ripoti iliyoandaliwa na Kamati ya pamoja ya mapitio ya kikatiba ya Bunge JCRC kuhusu kurekebisha kipengele cha 25 cha Katiba ili kuiruhusu serikali kutwaa ardhi bila fidia.

    Kwenye hati hiyo, bunge limesema AfriForum inajaribu kukwamisha mchakato wake wa kutunga sheria, na pia limeitaka mahakama ifute au kukataa ombi lililotolewa na AfriFroum, na kuitaka ilipe gharama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako