• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya waunga mkono makubaliano ya Brexit

    (GMT+08:00) 2018-11-26 09:09:41

    Umoja wa Ulaya umeridhia makubaliano kati yake na Uingereza kuhusu Uingereza kujitoa umoja wa Ulaya Brexit, kwenye mkutano maalum wa kilele uliofanyika jana mjini Brussels.

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claude Junker, amewaonya wanasiasa wa Uingereza wanaotaka kupinga makubaliano, akisema kama wanadhani wanaweza kupata makubaliano mazuri zaidi, basi watajuta muda mfupi baada ya kuyakataa. Amesema haya ni makubaliano pekee yanayowezekana.

    Viongozi wa nchi wanachama wa umoja wa Ulaya walipitisha waraka wenye kurasa 585 wa makubaliano ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya, pamoja na azimio la kisiasa kuhusu uhusiano kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya baada ya kujitoa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako