• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasimamisha safari za kuvuka mpaka baada ya maandamano ya wahamiaji Mexico

    (GMT+08:00) 2018-11-26 09:51:42

    Walinzi wa mpaka wa Marekani wamesimamisha safari zote za kuvuka mpaka kati ya mji wa San Diego na mji wa Tijuana, Mexico, wakati maelfu ya wahamiaji wanasongamana katika makazi ya muda kutoa maombi ya hifadhi.

    Ofisi ya Forodha na Ulinzi wa mipaka ya Marekani CBP mjini San Diego imesema, wahamiaji zaidi ya 1,800 wengi wakiwa wanatoka Honduras wamewasili Tijuana, mji wa mpakani nchini Mexico, na wengine zaidi wanatarajiwa kufika.

    Jumapili polisi huko Tijuana wameripotiwa kuvunja maandamano ya wahamiaji hao, na kusababisha hali ya waandamanaji kukimbia.

    Tukio hilo limekuja saa kadhaa baada ya rais Donald Trump wa Marekani kurudia onyo lake kwamba Marekani itafunga mpaka kati ya Marekani na Mexico kama kuna ulazima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako