• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yakabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa hatua madhubuti

  (GMT+08:00) 2018-11-26 16:48:45

  Mkutano mkuu wa 24 wa nchi zilizosaini makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa utafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao mjini Katowice, Poland, na nchi hizo zinatarajiwa kupiga kura ya maoni ili kupitisha utaratibu wa kutekeleza makubaliano ya Paris. Mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia mabadiliko ya hali ya hewa Bw. Xie Zhenhua amesema, China siku zote inakabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa msimamo imara na hatua madhubuti, na inatarajia mkutano huo utakamilisha mazungumzo kuhusu utaratibu wa kutekeleza makubaliano ya Umoja wa Mataifa.

  Mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia mabadiliko ya hali ya hewa Bw. Xie Zhenhua amesema, China ina matumaini matatu kuhusu mkutano utakaofanyika nchini Poland.

  "Kwanza, makubaliano ya Paris yalianza kufanya kazi mwaka 2015, kutokana na mpango uliowekwa, mkutano wa mwaka huu utakaofanyika mjini Katowice unapaswa kumaliza mazungumzo kuhusu utaratibu wa kutekeleza makubaliano hayo. Tunatumai kujenga utaratibu wa utekelezaji wa makubaliano ya Paris na makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Pili, tunatumai mazungumzo ya Talanoa yataendelea, ili kufahamisha uzoefu wa nchi mbalimbali katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Tatu, suala la bajeti linafuatiliwa na pande zote, tunatumai utekelezaji wa bajeti ya dola bilioni 100 za kimarekani utakaguliwa, ili kuweka msingi mzuri kwa ajili ya kutimiza malengo ya muda mrefu."

  Bw. Xie amesema China itakabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa msimamo imara na hatua madubuti, na kutekeleza makubaliano ya Paris. Anasema,

  "Tuliahidi kuwa hadi kufikia mwaka 2020, China itapunguza utoaji wa Carbon kwa asilimia 40 hadi 45, na nishati safi itachukua asilimia 15 ya nishati zote zinazotumiwa nchini China, na zaidi ya hayo, China itaongeza misitu kwa mita bilioni 1.3 za ujazo. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2017, China imepunguza utoaji wa Carbon kwa asilimia 46, kuongeza nishati safi hadi asilimia 13.8 ya nishati zote, na kuongeza misitu kwa mita bilioni 2.1 za ujazo. Hali hii imeweka msingi mzuri kwa ajili ya utimizaji wa malengo yote."

  Hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa pia zimehimiza maendeleo mazuri ya uchumi na jamii nchini China. Takwimu zinaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2005, matumizi ya nishati yaliyobanwa na China yanachukua zaidi ya asilimia 50 ya matumizi ya duniani.

  Bw. Xie amesisitiza kuwa nchi mbalimbali duniani zinapaswa kutekeleza makubaliano ya Paris kwa makini, na kutimiza malengo ya vipindi tofauti kwa kupitia ushirikiano wa kimataifa. Anasema,

  "Tunatumai nchi zilizoendelea zitatimiza ahadi zao kwa makini. Kutokana na kanuni ya makubalino ya Paris, nchi zilizoendelea zinapaswa kutoa misaada ya fedha na teknolojia kwa nchi zinazoendelea, ili kuziwezesha kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako