• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 25 wauawa katika mashambulizi ya mabomu katikati mwa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-11-26 18:32:00

    Watu 25 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa mapema leo baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la al-Shabab kulipua bomu lililotegwa kwenye gari na kuvamia nyumba ya imamu mmoja mjni Galkayo, katikati mwa Somalia.

    Ofisa wa polisi mjini humo Mohamed Abdi amesema, gari hilo liligonga geti la kituo hicho na wapiganaji hao kuingia ndani na kumuua Sheikh Abdiweli Ali Elmi na wafuasi wake.

    Habari zinasema, kundi hilo linamtuhumu Sheikh Abdiweli kwa kumtukana Mtume Mohammad.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako