• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya uchunguzi ya Zimbabwe yawataka wananchi wasizuie kuanzishwa kwake

    (GMT+08:00) 2018-11-26 19:39:24

    Tume ya kuchunguza vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi nchini Zimbabwe imewataka wananchi kuacha kulaumu uamuzi wa rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo wa kuanzisha tume hiyo pamoja na makamishna wake.

    Msemaji wa tume hiyo John Masuku amesema, wananchi wanapaswa kuthamini kuwa tume hiyo imeanzishwa kwa kufuata sheria ya nchi hiyo. Amesema ni vema ikafahamika kuwa rais Mnangagwa ameona ni vema kuteua makamishna wa sasa wa tume hiyo kutekeleza kazi hiyo ya kitaifa kwa kuendana na sheria za nchi.

    Taarifa ya tume hiyo imekuja baada ya wanaharakati kadhaa wa upinzani kulaumu kuanzishwa kwake na pia kutoa lawama kwa baadhi ya makamishna wa tume hiyo.

    Bw. Masuku pia amewataka polisi kuchunguza kikamilifu tuhuma zilizotolewa na mwandishi mmoja wa habari kuwa alishambuliwa vibaya katika mitandao ya kijamii na kutishiwa maisha baada ya kutoa ushahidi mbele ya Tume hiyo alhamis iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako