• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumai Uingereza na Umoja wa Ulaya zitafikia makubaliano ya mwisho kuhusu suala la Brexit

    (GMT+08:00) 2018-11-26 19:42:24

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, China inafuatilia suala la Brexit, na inatumai pande mbili za Uingereza na Umoja wa Ulaya zitafikia makubaliano ya mwisho kuhusu suala hilo.

    Bw. Geng Shuang amesema, Uingereza na Umoja wa Ulaya ni wenzi wa kimkakati wa pande zote wa China, na ustawi, utulivu na uwazi wa Umoja huo na Uingereza zinaendana na maslahi ya pande mbalimbali. Amesema sera ya China ya kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati yake na Uingereza na kati yake na Umoja wa Ulaya haitabadilika, na China inapenda kushirikiana na Umoja wa Ulaya na Uingereza kutoa mchango mpya kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako