Kenya na kampuni ya Huawei wanapanga kushirikiana kufuatilia ubora wa maji ili kuimarisha upatikanaji wa maji safi. Mkuu wa Mamlaka ya maji ya Kenya WRA Bw. Fred Nyongesa, amesema kwa sasa serikali inafanya majadiliano ya kusaini makubaliano na kampuni ya Huawei ili kuanza kusimamia ubora wa maji mwanzoni mwa mwaka kesho.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Huawei itaweka mifumo ya kusafirisha data kuhusu ubora wa maji kwa mamlaka ya maji ya Kenya, kutambua kama kuna bakteria wanaoweza kusababisha magonjwa, na kuimarisha usalama wa ikolojia ya maji (mito na maziwa).
Bw. Nyongesa amesema kwa sasa asilimia 60 ya maji yote ya ardhini kwenye maeneo ya mijini, na asilimia 40 ya maeneo ya maji vijijini yamechafuliwa, Mfumo huo mpya utaisaidia serikali kuwatambua moja kwa moja wanaochafua maji.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |