• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu na watunga sera wahimiza ongezeko lisilo na uchafuzi, na kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-11-27 08:55:48

    Wataalamu na watunga sera wanaokongamana mjini Kigali, Rwanda wametoa mwito kwa serikali za nchi za Afrika kutoa kipaumbele kwa ongezeko lisilo na uchafuzi na kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa.

    Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya ongezeko lisilo na uchafuzi duniani Bw. Frank Rijsberman, amesema ili kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa, nchi zinatakiwa kufikia asilimia 100 ya matumizi ya nishati endelevu, na kupunguza utoaji wa hewa zenye hatari, na kufuata mbinu za ujenzi zisizosababisha uchafuzi, na kufuata kilimo kinachohimili hali ngumu ya hewa.

    Bw. Rijsberman pia amesema nishati endelevu inaweza kusaidia kupunguza uchafuzi na kuongeza upatikanaji wa nishati safi, na kufanya ongezeko lisilo na uchafuzi na mkakati wa kuzoea mabadiliko ya hali ya hewa yawezekane.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako