• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mechi za nusu fainali ya Afrika kwa wanawake kurindima leo

    (GMT+08:00) 2018-11-27 08:57:13

    Michuano ya nusu fainali, kuwania taji la ubingwa bara la Afrika katika mchezo wa soka kwa upande wa wanawake, itachezwa leo Jumanne jijini Accra Ghana.

    Mechi ya kwanza itakuwa kati ya Cameroon na mabingwa watetezi Nigeria, huku Afrika Kusini nao watachuana na Mali. Cameroon na Mali, zilifuzu kutoka kundi A, baada ya kuwashinda wenyeji Ghana na Algeria.

    Nalo kundi B, liliongozwa na Afrika Kusini kwa alama saba, huku Nigeria ikimenyana na Nigeria kwa alama 6.

    Mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu, watafuzu kucheza katika kombe la dunia mwaka 2019 jijini Paris nchini Ufaransa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako