• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya kuogelea sasa Desemba

    (GMT+08:00) 2018-11-27 08:57:51
    Mashindano ya kuogelea kwa wachezaji chipukizi yamepangwa kufanyika Desemba 8 na 9 kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga jijini Dar es salaam.

    Katibu mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Inviolata Itatiro amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji chipukizi kuanzia miaka 12 kushuka chini, yana lengo la kuibua vipaji vya waogeleaji kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali nchini na ya kimataifa.

    Amesema kuwa kutakuwa na makundi manne, kundi la waogeleaji waliochini ya miaka saba, waogeleaji wa miaka nane na tisa, 10 na 11 na 12.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako