• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yatarajia kuanza kuuza nje mazao ya mifugo ifikapo mwaka 2040

    (GMT+08:00) 2018-11-27 09:32:30

    Waziri wa mifugo, uvuvi na maliasili ya wanyama wa Sudan Kusini Bw. James Duku amesema, nchi hiyo inatekeleza miradi 28 ya maendeleo ya mifugo ili kuinua ubora wa maliasili ya mifugo na kuanza kuuza nje mazao ya mifugo kabla ya mwaka 2040.

    Bw. Duku amesema, wizara yake itawekeza dola zaidi ya milioni 12.5 za kimarekani katika maendeleo ya miundombinu ya mifugo, ikiwemo machinjio, maabara na vituo vya kudhibiti maradhi.

    Pia amesema, Sudan Kusini ni maskani ya ng'ombe milioni 12 na mbuzi na kondoo zaidi ya milioni 28, lakini haijaweza kuuza mifugo yake kutokana na matishio yanayotokana na maradhi kama vile ugonjwa wa miguu na mdomo na homa ya bonde la ufa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako