• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa taifa wa China akutana na wawakilishi wa kudumu wa nchi wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2018-11-27 10:17:04

    Waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi jana hapa Beijing alikutana na ujumbe wa wawakilishi wa kudumu wa nchi wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

    Bw. Wang ameutaja Umoja wa Mataifa kama alama ya mfumo wa pande nyingi, amesisitiza kuwa pande zote zinatakiwa kushikilia kanuni za kimataifa ikiwemo madhumuni na kanuni za katiba ya Umoja wa mataifa ili kudumisha ukuaji mzuri wa utaratibu wa pande nyingi.

    Pia amesema, jumuiya ya kimataifa inautaka Umoja wa Mataifa kutoa mchango mkubwa zaidi, na kuwa na baraza la usalama linalobeba wajibu wa kuhakikisha usalama na utulivu wa kimataifa, na kulinda mfumo wa pande nyingi na kanuni za kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako