Waziri wa uchumi wa Ufaransa Bw. Bruno Le Maire ameonya kuwa maandamano ya hivi karibuni dhidi ya mpango wa kuongeza kodi ya mafuta ya petroli na dizeli yana athari mbaya kwa shughuli za kiuchumi za nchi hiyo. Amesema bado ni mapema kusema kama maandamano hayo yaitwayo "fulana ya njano" yanaathiri ukuaji wa uchumi, lakini viongozi wote wa biashara wamesema athari kwa shughuli za kiuchumi ni kubwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |