• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" watia nguvu mpya kwa maendeleo ya peninsula ya Iberian

  (GMT+08:00) 2018-11-27 17:26:04

  Kuhimizwa kwa ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kumeongeza biashara, maingiliano ya maslahi na mawasiliano ya watu kati ya peninsula ya Iberia na China, na pia kutia nguvu mpya kwenye maendeleo ya Hispania na Ureno zilizoko kwenye peninsula hiyo.

  Kwenye bandari ya Valencia nchini Hispania, meli moja kubwa inajazwa shehena. Saa kadhaa baadaye, meli hiyo ikiwa na bidhaa za nchi hiyo itafunga safari, na inatarajiwa kufika miji ya Qingdao na Shanghai, China baada ya siku 30.

  Mwaka jana, Kampuni ya Bandari ya Safari ya Baharini ya Zhongyuan ya China ilinunua asilimia 51 ya hisa ya Kampuni ya Bandari ya NPH ya Hispania, na kupata mamlaka ya kuendesha vituo vya shehena vya bandari za Valencia na Bilbao, na reli za Madrid na Zaragoza. Hispania inafurahia uwekezaji wa China, na kutarajia mafanikio ya pamoja. Mwenyekiti wa idara inayoshughulikia mambo ya bandari ya Bilbao ya Hispania Bw. Ricardo Barkala anasema,

  "Kwa dunia nzima, pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni fursa kubwa yenye maana ya kiuchumi na kihistoria, haswa kwa biashara ya kimataifa. Kama bandari za Hispania zikiwa daraja la kuunganisha Asia na Ulaya, tutakuwa na njia nyingine ya kuongeza biashara na China."

  Meneja mkuu wa Kampuni ya Bandari ya NPH Bw. Sun Kai amesema, kampuni hiyo itaijenga bandari ya Valencia iwe bandari kuu ya sehemu ya magharibi ya bahari ya Mediterranean, ili kuhudumia biashara kati ya nchi husika na "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Anasema,

  "Hakuna bandari kuu katika sehemu ya magharibi ya bahari ya Mediterranean, bandari ya Valencia pamoja na bandari ya Bilbao katika siku za baadaye ni chaguo zuri. Ikiwa nchi ya tano kwa ukubwa wa uchumi katika Umoja wa Ulaya, Hispania imedumisha asilimia 3 ya ongezeko la uchumi katika miaka mitatu iliyopita. Shughuli zetu ni nini? Shughuli zetu ni kuhudumia biashara."

  Katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano halisi kati ya China na Hispania katika sekta mbalimbali umepiga hatua kubwa. Mbali na bandari, kampuni za nchi hizo mbili pia zimeshirikiana katika kupanua soko la nchi nyingine. Kwa mfano Kampuni ya SINOPEC ya China kwa kushirikiana na kampuni ya Hispania, zilifanikiwa kupata mradi wa usafishaji wa mafuta wa Kuwait.

  Aidha, reli ya kuunganisha mji wa Yiwu, China na mji wa Madrid, Hispania imekuwa njia muhimu nyingine ya kuunganisha Asia na Ulaya. Tangu mwaka 2014, jumla ya treni 483 zimesafirisha makontena elfu 46.4 kutoka Yiwu kwa Madrid, na treni 137 zimesafirisha makontena 7,120 kutoka Madrid kwa Yiwu.

  Hali kadhalika, katika miaka ya hivi karibuni, Ureno ambayo pia iko katika peninsula ya Iberia imepata mafanikio makubwa katika kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na China. Hadi sasa, kampuni za China na wachina binafsi wamewekeza zaidi ya Euro bilioni 9 nchini Ureno. Waziri wa mambo ya nje wa Ureno Bw. Augusto Santos Silva anasema,

  "Kwa upande wa Ureno, tunaweza kuongeza thamani ya bandari zetu kutokana na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kutumia mawasiliano ya barabara na Hispania kwa ufanisi zaidi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako