• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu zaidi laki 3 nchini Afghanistan wakimbia makazi yao kutokana na mgogoro katika mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-11-27 18:20:33

    Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinadamu (OCHA) imesema watu zaidi laki 3 wamekimbia makazi yao kutokana na mgogoro katika mwaka huu nchini Afghanistan.

    Ripoti iliyotolewa jana na ofisi hiyo nchini Afghanistan imesema, vita inayoendelea nchini humo, hali ya usalama inayozidi kuwa mbaya na vurugu zinazoendelea zimewalazimu watu kukimbia makazi yao na kwenda sehemu zenye usalama.

    Lakini ofisi hiyo pia imesema idadi hiyo ya watu waliokimbia makazi yao imepungua kwa asilimia 37 kuliko mwaka jana wakati kama huu ambayo ilifikia laki 4.81.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako