• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema kitendo chochote cha kuharibu urafiki kati ya China na Pakistan hakitafanikiwa

    (GMT+08:00) 2018-11-27 18:40:25

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, kitendo chochote kinacholenga kuharibu urafiki kati ya China na Pakistan hakitafanikiwa, na China itaendelea kuwasiliana na Pakistan kuhusu utatuzi wa shambulizi dhidi ya ubalozi wa China mjini Karachi.

    Amesema China inaamini Pakistan ina uwezo wa kulinda usalama na utulivu wa ndani na kuchukua hatua kudumisha maslahi, usalama wa wachina na kampuni za China nchini humo.

    Bw. Geng pia amesema, utatuzi wa tukio hilo umeonesha urafiki na nia ya dhati za watu wa nchi hizo mbili za kuaminiana na kusaidiana, na kuthibitisha tena urafiki imara na uhusiano wa siku zote wa wenzi wa kimkakati kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako