• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EAC kuandaliwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-11-27 18:42:59
    Mkutano wa 20 wa wakuu wan chi za Afrika Mashariki utaandaliwa jijini Arusha Ijumaa ya tarehe 30 mwezi huu. Mojawapo ya agenda kuu zitakazojadiliwa kwenye kongamano hilo ni kupitisha itifaki mbalimbali.

    Aidha mkutano huo utatoa fursa mwafaka ya kupitia ripoti ya awali yenye mapendekezo ya nchi za Ukanda wa Afrika Mashari kujiundia magari yao wenyewe. Hili itasaidia kupunguza idadi ya magari yanayoagizwa kutoka mataifa ya nje. Vile vile, viongozi hawa watajadiliana kwa kina jinsi ya kuboresha viwand avya ngozi na pamba. Lengo kuu likiwa kupunguza uagizaji wa bidhaa hizi kutoka nje.

    Vile vile mkutano huwa utapitisha kuwa sheria miswada mbalimbali ambayo imejadiliwa na kupitishwa na Bunge la Jumuiya ya afrika Mashariki (EALA). Miswada hiyo ni kama vile kuthibiti bidhaa za nailoni, ambao ni mswada wa mwaka wa 2016. Halikadhalika muswada wa kuanzishwa Taasisi ya Fedha nchi za Ukanda wa Afrika ya Mashariki (EAC) ya mwaka 2018 miongoni mwa miswada mingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako