• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dar Es Salaam : Uber na Taxify zamulikwa

    (GMT+08:00) 2018-11-27 18:43:56
    Baadhi ya wateja wanaotumia usafiri wa magari ya Uber na Taxify jijini Dar es Salaam, wamewasilisha malalamishi yao dhidi ya madereva matapeli wa huduma hizi za usafiri. Wateja hawa wanasema kwamba madereva wa Uber na Taxify wamekuwa wakiwalaghai kwa kuwalipisha pesa za ziada kwa kuongeza mwendo wa usafiri. Hii huenda ikaathiri biashara ya uber na Taxify kutokana na wateja kukosa imani kwao.

    Wakurugenzi wakuu wa huduma hizi za usafiri wamekiri kuwa wamepata malalamishi na kwamaba wameanza kuyashughulikia. Wasafiri wameombwa kuripoti visa vya ulaghai wa madereva wa Uber na Taxify ili madereva hao kuchukuliwa hatua. Visa hivi vimeripotiwa sana nchini Kenya na sasa vimepenyeza Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako