• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Sekta ya maua mashakani

    (GMT+08:00) 2018-11-27 18:44:14

    Hali ya wasiwasi imeanza kushudiwa katika sekta ya maua kote nchini Kenya. Hii ni baada ya kukosekana kwa mbole amaalum ya maua, jambo ambalo huenda likasababisha maelfu ya wakenya kupoteza ajira. Mkurugenzi mkuu wa Baraza la Maua nchini Kenya Clement Tulezi, anasema kwamba hali hii imekuwa mbaya zaidi miezi mitano iliyopita.

    Juhudi za kutatua zimeambulia patupu. Kwa sasa, wahusika wakuu wa serikali wameombwa kuingilia kati swala hili, ambalo linatishia kuwapora wakenya 150,000 ajira zao. Ukosefu wa mbolea hii imeathiri sana idadi ya maua yanayosafirishwa kwenye mataifa ya nje.

    Hata hivyo, serikali imenunua mbolea ambayo kwa sasa inafanyiwa vipimo na Shirika la ubora wa Viwango vya Bidhaa (KBS).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako