• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa makala kwenye gazeti la ABC la Hispania

    (GMT+08:00) 2018-11-27 20:29:40

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa makala kwenye gazeti la ABC la Hispania yenye kichwa cha "kuingia kwenye zama mpya na kushirikiana kupata ustawi mpya".

    Rais Xi amesema, moja ya majukumu yake katika ziara yake ni kujadiliana na viongozi wa nchi alizozuruna viongozi wa makundi makuu ya kiuchumi duniani kuhusu namna ya kuimarisha mshikamano wa jamii ya kimataifa, kukamilisha usimamizi wa dunia, kuendeleza uhusiano wa kiwenzi, kuzidisha urafiki na ushirikiano, na kuhimiza amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa dunia.

    Amesema historia inaonyesha kuwa, utamaduni wa China na Hispania unalingana na kuvutia kila upande, maendeleo, maingiliano na kujiendeleza kwa pamoja. Tangu mwaka 1973 nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, pande hizo zinaheshimiana, kutendeana kwa usawa, kushirikiana kwa kunufaishana, na kuhimiza uhusiano kati yao kuendelea kwa utulivu.

    Pia amesema anatumai kupitia ziara yake hiyo, kushirikiana na viongozi wa Hispania kuenzi urafiki kati ya China na Hispania, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, ili kujenga mustakabali mzuri zaidi wa uhusiano kati ya China na Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako