• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Tabu ipo pale pale: Mbappe, Neymar warejea kuivaa Liverpool

    (GMT+08:00) 2018-11-28 08:52:02

    Inaonekana klabu ya PSG inaelekea kushinda vita ya kuhakikisha nyota wao Kylian Mbappe na Neymar Jr wanakuwa fit kuivaa Liverpool katika mechi ya kundi C ya ligi ya mabingwa Ulaya inayotarajiwa kupigwa leo Jumatano, baada ya wawili hao kufanya mazoezi na wenzao jana.

    Nyota hao wa kimataifa wa Brazil na Ufaransa walishindwa kumaliza mechi za kirafiki za nchi zao wiki iliyopita baada ya kupata maumivu yaliyopelekea kuzuka kwa hofu kubwa klabuni kwao kuwa labda wangeweza kukosa mechi hiyo muhimu ya UCL.

    vipimo vya mwisho vilivyofanywa Ijumaa hii vilitoa majibu kuwa Neymar ana asilimia 50 ya kucheza mechi hiyo huku Mbappe yeye akionekana kuwa kamili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako