• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaahidi kuwasaidia wawekezaji wa China kuanzisha kituo nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2018-11-28 08:56:02

    Serikali ya Kenya imeahidi kuwasaidia wawekezaji wa China kutoka mkoani Zhejiang kuanzisha kituo chao nchini Kenya. Katibu mkuu wa viwanda, Biashara na Ushirika Bibi Betty Maina, amesema kwenye kongamano la biashara mjini Nairobi, kuwa Kenya inawatambua wawekezaji kutoka China kama wadau muhimu kwenye safari ya Kenya kufikia maendeleo ya kiuchumi.

    Ujumbe wa makampuni zaidi ya 50 kutoka mkoa wa Zhejiang uko nchini Kenya kutafuta fursa za uwekezaji na makubaliano ya kibiashara kwenye maeneo ya usindikaji wa chakula, nguo, bidhaa za ngozi, ujenzi, magari na sekta ya uchukuzi wa baharini.

    Bibi Maina amesema wawekezaji wa China wanaweza kutoa mchango mkubwa kwenye utekelezaji wa ajenda ya Big four ya Rais Uhuru Kenyatta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako