• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Afrika Kusini lapitisha sheria ya kupambana na uhalifu wa kimtandao

    (GMT+08:00) 2018-11-28 08:59:05

    Bunge la Afrika Kusini limepitisha sheria ya kupambana na makosa ya kimtandao, yenye lengo la kupambana na ongezeko la uhalifu wa kimtandao.

    Msemaji wa Bunge Bw. Moloto Mothapo amesema lengo kuu la sheria hiyo ni kuharamisha usambazaji wa ujumbe wenye madhara, na sheria hiyo inatoa amri za ulinzi wa muda na kutaka kusimamia madaraka ya kuchunguza uhalifu wa kimtandao.

    Kutokana na sheria hiyo mtu yeyote atakayehusika na uhalifu wa kimtandao, anaweza kuhukumiwa kifungo cha kati ya mwaka mmoja na miaka 15, kutokana na ukubwa wa kosa alilofanya.

    Afrika Kusini ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na matukio mengi ya uhalifu wa kimtandao, unaosababisha kupotea kwa dola milioni 159 za kimarekani kila mwaka. Sheria hii inazipa mahakama mamlaka ya kuchukua hatua kwenye baadhi ya matukio ambayo hayakuwekwa wazi kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako