• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yahimiza shughuli za uchumi wa majini ili kuhimiza usalama wa chakula barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-11-28 08:59:26

    Shughuli za uchumi wa majini Afrika zimetajwa kuwa zinaweza kuwa na mchango mkubwa katika kupunguza njaa na utapiamlo, wakati mazao ya kilimo yanapungua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kupungua kwa eneo la ardhi inayolimika.

    Mkurugenzi wa idara ya uvuvi na kilimo cha majini ya Shirika la chakula la kilimo la Umoja wa Mataifa FAO Bw. Manuel Barange, amesema mjini Nairobi kwenye ufunguzi wa kongamano la kilele kuhusu uchumi wa bahari, kuwapa motisha wakulima wadogowadogo wa Afrika kuhusisha na ufugaji wa samaki kutaongeza usalama wa chakula na kipato chao.

    Bw. Barange amesema ili sekta ya ufugaji samaki mdogo mdogo ifanye kazi, serikali zinatakiwa kuongoza mnyororo wa thamani yake, ili kupunguza hasara zinazoweza kutokea baada ya mavuno.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako