• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yatangaza siku moja ya maombolezo kwa wahanga wa ajali ya boti

    (GMT+08:00) 2018-11-28 09:07:40

    Serikali ya Uganda imetangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa kwa wahanga wa ajali ya boti iliyotokea wikiendi iliyopita kwenye ziwa Victoria.

    Naibu wa kwanza wa waziri mkuu wa Uganda Bw. Moses Ali ameliambia bunge kuwa Ijumaa ijayo itachukuliwa kuwa ni siku ya maombolezo ya kitaifa kwa watu waliofariki dunia baada ya boti moja kupinduka Jumamosi karibu na kisiwa cha Mutima kwenye wilaya ya kati ya Mukono.

    Wabunge wa Uganda jana walitoa heshima kwa watu zaidi ya thelathini waliofariki katika ajali hiyo, baadhi yao waliilaumu serikali kwa kushindwa kuchunguza ubora wa boti hiyo.

    Kwa mujibu wa jeshi la Uganda, miili ya watu 35 imepatikana na wengine 27 waliokolewa. Boti iliyokumbwa na ajali ilikuwa inasafari kutoka Port Bell Luzira mjini Kampala kwenda Kisiwa cha Mutima, ikiwa ni abiria zaidi ya 120, ambayo ni zaidi ya uwezo wake wa kubeba watu 100.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako