• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji katika nishati mbadala watajwa kuhimiza ukuaji wa uchumi Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-11-28 09:07:57

    Mtaalamu wa nishati wa Nigeria amesema uwekezaji mkubwa katika nishati mbadala utakuwa ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya viwanda na ukuaji wa uchumi nchini Nigeria.

    Bw. Yemi Kolawole amewaambia wanahabari kuwa mbali na kuhimiza mahitaji ya nishati, nishati mbadala inafaa kwa uchumi wa Nigeria ambayo ni moja kati ya chumi kubwa zaidi barani Afrika, kwa kuwa pia haina madhara kwa mazingira ya asili.

    Bw. Kolawole amesisitiza kuwa kuwekeza fedha zaidi katika nishati endelevu ni mbinu sahihi ya kutatua mahitaji ya nishati nchini Nigeria.

    Serikali ya Nigeria imesema inalenga kukidhi asilimia 30 ya mahitaji yake ya nishati kwa kutumia nishati endelvu, ili kuwe na vyanzo anuwai vya nishati nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako