• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping akutana na mfalme Felipe wa sita wa Hispania

    (GMT+08:00) 2018-11-28 10:30:34

    Rais Xi Jinping wa China ameanza ziara nchini Hispania na kukutana na mfalme Felipe wa Sita wa Hispania katika kasri la Zarzuela mjini Madrid. Rais Xi amesema, uhusiano kati ya China na Hispania uko katika kipindi kizuri zaidi, na anatarajia ziara yake itaimarisha urafiki, kuinua kiwango cha ushirikiano na kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, China inapenda kuendelea kuungana mkono Hispania katika masuala yanayohusisha maslahi makuu ya kila upande na yale wanayofuatilia kwa pamoja. Pande hizo mbili zinapaswa kuongeza ushirikiano katika sekta za biashara, utalii, soko la upande wa tatu ndani ya utaratibu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ili kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Hispania ufikie kwenye ngazi mpya katika karne mpya na kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

    Mfalme Felipe wa sita amesema wakati Hispania na China zinaadhimisha miaka 45 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, Hispania inapenda kuendelea kudumisha mawasiliano ya karibu na China, kuinua kiwango cha ushirikiano wa kivitendo, kuongeza mawasiliano na uratibu katika mambo ya kimataifa, na kusaidia kuimarisha uhusiano kati ya Ulaya na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako