• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iko tayari kushirikiana na Ujerumani kuimarisha ushirikiano wa pande mbili

    (GMT+08:00) 2018-11-28 17:19:01

    Naibu waziri mkuu wa China Liu He ambaye yuko ziarani nchini Ujerumani amesema, China iko tayari kufanya kazi na Ujerumani ili kuinua ushirikiano wa pande mbili kwenye maeneo ya fedha, biashara na uwekezaji.

    Liu amesema hayo alipotoa hotuba wakati wa halfa ya kufunga mkutano wa 8 wa Hamburg wenye kaulimbiu ya "China yakutana na Ulaya". Amesema China iko tayari kufanya kazi na Ujerumani kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili.

    Naibu waziri huyo pia aliwasilisha ujumbe wa rais Xi Jinping wa China kwa Kansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel, ambapo rais Xi amesema China na Ujerumani ni wenzi wa kimkakati wa pande zote, na ushirikiano wa pande hizo mbili katika Nyanja mbalimbali umepata maendeleo makubwa.

    Bi. Merkel amesema Ujerumani imeweka umuhimu mkubwa katika kuendeleza uhusiano wa pande mbili na China na maslahi yake katika ushiriki wake kwenye pendekezo la China la Ukanda Mmoja na Njia Moja. Ameongeza kuwa Ujerumani daima inakaribisha na inaunga mkono kikamilifu wawekezaji kutoka China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako