• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 22 wafariki baada ya lori lililobeba kemikali kulipuka kaskazini mwa China

    (GMT+08:00) 2018-11-28 17:19:26

    Watu 22 wamefariki na wengine 22 kujeruhiwa baada ya lori lililobeba kemikali kulipuka wilayani Qiaodong, mjini Zhangjiakou, mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China mapema leo na kusababisha magari yaliyokuwa karibu kuwaka moto.

    Wizara inayosimamia mambo ya dharura imepeleka kikosi kazi katika eneo la tukio ili kuongoza kazi za uokoaji, huku serikali ya mkoa huo ikihakiki utambulisho wa watu waliofariki.

    Mlipuko huo ulisababisha malori 38 na magari 12 yaliyokuwa karibu kuwaka moto.

    Kazi ya uokoaji na uchunguzi zaidi bado vinaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako