• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya mwaka 2018 kuhusu utafiti wa mambo ya walemavu ya China yatolewa

    (GMT+08:00) 2018-11-28 17:29:09

    Ripoti ya mwaka 2018 kuhusu utafiti wa mambo ya walemavu ya China imetolewa leo hapa Beijing ikiwa na sehemu sita zikiwemo ripoti ya jumla ya maendeleo ya mambo ya walemavu ya China, jumuiya ya walemavu, na afya ya walemavu.

    Ripoti hiyo inasema, mwaka 2017 China ilipata mafanikio katika kuhimiza maendeleo ya mambo ya walemavu. Takwimu zinaonyesha kuwa, watu zaidi ya laki 7 wenye ulemavu wamepata mafunzo ya kiufundi mwaka jana, walemavu elfu 21 walioko vijijini wamepata msaada wa mipoko isiyo na riba, na walemavu zaidi ya laki moja wamepata ajira katika vituo vya kuwasaidia walemavu kuondokana na umaskini.

    Katika huduma ya jamii, utaratibu wa ruzuku ya maisha kwa walemavu wenye hali duni kiuchumi na ruzuku ya huduma ya afya kwa walemavu umetekelezwa kote nchini, na kunufaisha walemavu zaidi milioni 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako