• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapenda kushirikiana na pande mbalimbali kufanikisha mkutano ujao wa G20

  (GMT+08:00) 2018-11-28 18:50:39

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inatarajia kundi la G20 litaendelea kutia nguvu kwenye maendeleo endelevu ya uchumi wa dunia.

  Bw. Geng amesema, hivi sasa, uchumi wa dunia unakabiliwa na hatari ya kudidimika na athari ya mfumo wa upande mmoja na vitendo vya kujilinda. China inatarajia mkutano wa G20 utapata mafanikio katika kulinda mfumo wa pande nyingi, kuhimiza ushirikiano wa wenzi, na kuboresha usimamizi wa uchumi wa dunia. Pia katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuongeza ongezeko la uvumbuzi na kusukuma mbele maendeleo ya pamoja.

  Bw. Geng pia amesema, China inapenda mkutano huo upate mafanikio ili kuhimiza ongezeko la uchumi wa dunia na maendeleo ya usimamizi wa uchumi wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako