• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Ushelisheli zinalenga kuimarisha ushirikiano wao kwa kushirikiana zaidi katika eneo la uchumi wa rasilimali za majini.

    (GMT+08:00) 2018-11-28 19:05:07
    Kenya na Ushelisheli zinalenga kuimarisha ushirikiano wao kwa kushirikiana zaidi katika eneo la uchumi wa rasilimali za majini.

    Rais wa Ushelisheli Danny Faure na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wamekubaliana kuhusu hilo,jamabo ambalo pia linapewa umuhimu mkubwa katika kongamano la kwanza la Uchumi Endelevu wa Rasilimali za Majini unaoendelea katika jumba la mikutano la KICC jijini Nairobi.

    Taarifa katika tovuti ya Ikulu ya Ushelisheli imesema kuwa viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu maeneo mengine yenye maslahi ya pamoja na kuelezea maslahi yenye nguvu na kujitolea kwa nguvu kwa nchi zote mbili ili kuendeleza mahusiano na ushirikiano wao.

    Ushelisheli imeikumbatia dhana ya Uchumi wa rasilimali za majini kama utaratibu wa kutambua maendeleo endelevu ya kiuchumi yanayotokana na uchumi wa bahari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako