• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania John Magufuli ameipongeza China kwa kutoweka masharti yoyote wakati inapotoa msaada wa kifedha.

    (GMT+08:00) 2018-11-28 19:14:14
    Rais wa Tanzania John Magufuli ameipongeza China kwa kutoweka masharti yoyote wakati inapotoa msaada wa kifedha.

    Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana katika uzinduzi wa maktaba ya kisasa iliyojengwa kwa msaada wa fedha za China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

    Alisema ingekuwa ni washirika wengine wa maendeleo,watanzania wangelazimishwa kutembea kwa migongo yao ili wapate msaada huo.

    Aliongeza kuwa China ni rafiki wa kweli kwa kuwa imetoa msaada huo wa maktaba bila ya malipo yoyote.

    Maktaba hiyo ya kisasa na kituo cha mikutano kimejengwa na China kwa gharama ya $40 milioni (zaidi ya Tsh92 bilioni).

    Kauli hiyo ya Magufuli imetolewa wakati kuna washirika kadhaa wa maendeleo hivi karibuni walitangaza kusistisha au kupitia upya mipango ya usaidizi kwa Tanzania kutokana na sera mbalimbali za serikali na kile wanachokitaja kuwa ni malalamiko kuhusu uongozi,demokrasia na haki za binadamu.

    Wafadhili hao ,wakiwemo Umoja wa Ulaya,Benki ya Dunia,na nchi ya Denmark wamedokeza kuwa utoaji wa msaada kwa Tanzania siku za baadaye utapitia masharti kadhaa.

    Serikali ya Rais Magufuli imekuwa ikitafuta mikopo ya ujenzi wa miundombinu mikubwa kutoka China ili iweze kujenga sehemu ya reli ya kisasa.

    Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania imechukua mikopo ya $2.347 bilioni kutoka China katika kipindi cha kati ya mwaka 2000 na 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako