• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China nchini Rwanda aahidi kuitafutia soko kahawa ya Rwanda nchini China

    (GMT+08:00) 2018-11-28 19:15:53

    Balozi wa China nchini Rwanda,Bw Henry Rao Hongwei,amewahakikishia wazalishaji wa kahawa na chai nchini Rwanda upatikanaji wa soko la mazao yao katika nchi ya China.

    Bw Hongwei aliyasema hayo jana wakati wa ziara katika kiwanda cha kuchoma kahawa cha Rwanda Coffee farmers kilichoko katika makao makuu ya Bodi ya Kitaifa ya maendeleo ya mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo jijini Kigali.

    Ziara hiyo ambayo imekuja baada ya mkataba wa biashara uliotiwa saini hivi karibuni kati ya Rwanda na kampuni ya China ya Alibaba,unaolenga kusafirisha kahawa ya Rwanda nchini China.

    Balozi Hongwei aliahidi kuvutia wawekezaji wengi zaidi nchini Rwanda kwa kuwapatia habari kuhusu fursa zinazopatikana katika sekta hiyo.

    Kahawa nchini Rwanda inakuzwa na wakulima 355,000 katika ardhi ya hekta 37,000 huku uzalishaji wa kahawa kwa mwaka ukiwa kati ya tani mjazo 16,000 na 21,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako