• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa uchumi wa Baharini wataka hatua za kudhibiti tafiti zisizopangwa za mafuta baharini

    (GMT+08:00) 2018-11-28 19:51:10

    Washiriki wa Mkutano wa Uchumi Endelevu wa Baharini unaofanyika jijini Nairobi, Kenya, wametaka mpango sahihi ufanyike ili kuhakikisha utafiti wa mafuta na gesi baharini hauathiri viumbe wa baharini.

    Waziri wa Nchi katika ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira kutoka Tanzania Bw. January Makamba amesema, mpango sahihi na matumizi ya sera sahihi ili kutafuta rasilimali baharini ni muhimu katika kulinda utajiri mkubwa wa asili ulioko baharini. Amesema kuna haja ya sheria na kanuni za kimataifa kuhusu jinsi ya kuendeleza na kutumia vizuri rasilimali zinazopatikana baharini, na jinsi mafuta yaliyoko baharini yanaweza kutolewa na kusafirishwa.

    Naye mkurugenzi wa Idara ya Takwimu na Habari za Baharini iliyo chini ya Wizara ya Maliasili ya China Bw. He Guangshun amesema, China itachangia mafanikio yake katika kuendeleza uchumi wa baharini ili kuboresha ushirikiano wa kimataifa katika maeneo yanayohusiana na ajenda ya kijani, usalama wa chakula, na amani na utulivu. Amesema China imetoa kipaumbele kwa mafanikio ya ushirikiano wa uchumi wa baharini unaoendana na pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako