• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atoa makala kwenye gazeti la Argentina

  (GMT+08:00) 2018-11-28 21:14:54

  Rais Xi Jinping wa China ambaye yupo ziarani nchini Argentina na kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kundi la nchi 20 (G20) leo ametoa makala kwenye gazeti la Horn la nchi hiyo.

  Kwenye makala hiyo rais Xi amesisitiza kuwa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita, China na Argentina zinapaswa kushirikiana kuanzisha zama mpya ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote, ili kunufaisha wananchi wao. Amependekeza nchi hizo mbili kuongeza mawasiliano ya kimkakati na kufuata kanuni ya kuheshimiana na kuaminiana, kuzidisha ushirikiano halisi ili kutimiza mafanikio ya pamoja, kukuza mawasiliano ya watu ili kuelimishana, kuongeza uratibu na ushirikiano na kuendelea kusaidiana.

  Aidha, rais Xi ameihimiza G20 kuongoza maendeleo ya uchumi wa dunia, na kusukuma mbele mchakato wa maendeleo ya utandawazi wa uchumi duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako